TAMASHA LA KIMATAIFA LA JULIUS KAMBARAGE NYERERE

8
:
88
:
88
:
88

 

K

Tamasha la Kimataifa la Julius Kambarage Nyerere (JUKANYE)

Jasiri Arts & Culture Institution (JACI), yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam na iliyosajiliwa chini ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), ni taasisi inayojihusisha na maendeleo ya sanaa, utamaduni na uratibu wa matukio ya kijamii na kihistoria. Kwa kushirikiana na CATZ Company Limited, yenye makao yake jijini Dar es Salaam na iliyosajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Namba ya Usajili 173701225, kampuni inayojishughulisha na ubunifu, uandishi na uzalishaji wa maudhui ya kijamii na kiutamaduni, pamoja na Makumbusho ya Taifa la Tanzania (NMT)—taasisi ya umma iliyo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, yenye jukumu la kuhifadhi, kulinda na kuendeleza urithi wa kihistoria wa Tanzania—wanafuraha kutangaza kuanza rasmi kwa maandalizi ya Tamasha la Kimataifa la Julius Kambarage Nyerere (JUKANYE) 2027, tamasha la kimataifa linalofanyika kila baada ya miaka miwili kwa lengo la kuenzi maisha, urithi, falsafa na maadili ya kudumu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania.

Tamasha hili linaandaliwa kwa ushirikiano wa karibu na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika (African Liberation Heritage Centre – ALHC) pamoja na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).

 

JUKANYE 2027 itafanyika katika Viwanja vya Kisongo, Mkoa wa Arusha, Tanzania, kuanzia tarehe 17 Julai hadi 1 Agosti 2027.

 

Tamasha litajumuisha shughuli mbalimbali zikiwemo:

 

Kukuza na Kutangaza Utalii

Maonesho ya Kimataifa na Maonesho ya Biashara

Maonesho ya Utamaduni na Urithi wa Taifa

Mikutano, Makongamano na Warsha

Michezo na Shughuli za Burudani

Maonesho ya Sanaa, Utamaduni na Burudani

Huduma za Kijamii na Uhamasishaji wa Jamii

Mitandao ya Biashara na Uwekezaji

Maonesho ya Ubunifu na Sekta za Uchumi Bunifu

Hafla ya Utambuzi na Utoaji wa Tuzo

 

JUKANYE ni jukwaa la kimataifa linalokusanya pamoja serikali, taasisi za utamaduni, washirika wa maendeleo, wawekezaji, wafanyabiashara, wasanii, watafiti, vijana na jamii kutoka Tanzania, Afrika na sehemu mbalimbali duniani ili kusherehekea urithi wa Afrika, kuimarisha umoja wa Waafrika, kukuza utalii endelevu, kuhamasisha biashara na uwekezaji, pamoja na kuhamasisha kizazi cha sasa na kijacho kupitia urithi na maono ya kudumu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Tamasha hili pia linalenga kuitangaza Tanzania kama kitovu cha utalii wa urithi, utamaduni, diplomasia ya utamaduni, ubunifu na maendeleo endelevu barani Afrika.

uhusu Tamasha la Jukanye 2026

JUKANYE International History Festival ni tamasha la kipekee linaloratibiwa na Jasiri Arts & Culture Institution (JACI) kwa kushirikiana na CATZ Company Ltd, likiwa sehemu ya mpango wa miaka 10 wa kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Lengo lake kuu ni kuenzi urithi wa ukombozi wa Afrika, kukuza uzalendo, kuunga mkono juhudi za utalii na utamaduni wa Tanzania, sambamba na kusisitiza mshikamano wa Waafrika katika kuujenga uchumi wa bara letu.

Tamasha hufanyika kila baada ya miaka miwili, na toleo la kwanza litafanyika Arusha, Tanzania kuanzia 01–13 Septemba 2026, likihusisha Utalii maonyesho, warsha, mijadala, burudani, na utoaji tuzo.

 

Kauli mbiu: “Uchumi wa Afrika utaimarishwa na Waafrika wenyewe kwa kushikamana.”

 

Wabeba maono ya Jukanye

Ahmad Hussein Mwita - JACI

Mwanzilishi wa wazo la JUKANYE Festival

 

Mzalendo, mweledi wa sanaa, na mtetezi wa historia ya ukombozi wa Afrika. naamini kuwa kizazi cha sasa kinapaswa kurithi na kuenzi urithi wa mashujaa wetu.

Mainda Mkwiro - JACI

Mwanzilishi Mwenza wa Tamasha la Jukanye.


Sauti ya urithi, lenzi ya utambulisho.
Akiangazia roho ya taifa katika hadithi zinazohamasisha, kuhifadhi, na kuamsha.

Mwene Jabril Ikaweba - JACI

Mwanzilishi Mwenza wa Tamasha la Jukanye.

JUKANYE si tamasha tu – ni jukwaa la ukombozi wa fikra za Kiafrika. Ni mwito wa kizazi chetu kutetea historia yetu, lugha yetu, na hadhi ya bara letu.

Silondwa C. Johns - CATZ

 Mwandishi wa Program ya Jukanye

 

JUKANYE si tamasha tu - ni moto wa mababu zetu uliorejea. kuamsha kumbukumbu ya Afrika,
Kuandika fahari yake, na kupandisha utukufu wa africa jukwaani.

Wajumbe wa Bodi:

Majukumu

 

  • Kuratibu Mialiko Rasmi:

  • Kuandaa na kutuma mialiko kwa wageni wa heshima wakiwemo viongozi wa kitaifa na kimataifa, mabalozi, mashujaa wa ukombozi, wasanii, na wadau wakuu wa tamasha.

  • Kuhakikisha Itifaki Inazingatiwa:

  • Kuratibu mapokezi ya wageni maalum kwa kufuata taratibu za heshima na hadhi zao.

  • Kuhakikisha taratibu za kitaifa na kimataifa za itifaki zinafuatwa ipasavyo kwenye hafla rasmi.

  • Kurahisisha Uratibu wa Wageni Maalum:

  • Kupanga ratiba, usafiri, malazi, na ulinzi wa wageni mashuhuri wanaoshiriki tamasha.

  • Kuwapa taarifa muhimu wageni kuhusu programu ya tamasha na mahitaji yao binafsi.

  • Kuhakikisha Uwasilishaji Bora wa Hotuba na Heshima:

  • Kusimamia mpangilio wa hotuba, utoaji wa tuzo, na matukio mengine ya hadhi ya juu.

  • Kuandaa watangazaji au wahudumu wa hafla wenye uelewa wa lugha na mila za itifaki.

  • Kuwezesha Ushirikiano wa Kimataifa:

  • Kufanikisha ujio na ushiriki wa wageni kutoka nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kusaidia utoaji wa viza na taarifa za kiusalama na mahitaji maalum.

KAMATI

 

 

A). KAMATI KUU YA MAANDALIZI (STEERING COMMITTEE)

 

1. Mwenyekiti  
Msimamizi Mkuu wa Tamasha, atasimamia na kuongoza, mwelekeo na utekelezaji wa majukumu yote.
🔹Ataratibu vikao na kuhakikisha kila kamati inafanya kazi kwa ufanisi.

 

2. Makamu Mwenyekiti 
Msaidizi wa Mwenyekiti, anachukua nafasi wakati Mwenyekiti hayupo na kusimamia utekelezaji wa maamuzi.

 

3. Katibu wa Kamati Kuu 
Anasimamia maandalizi ya mikutano, uchapaji wa nyaraka, na mawasiliano rasmi.

 

4. Mhazini 
Anasimamia mapato na matumizi ya fedha za tamasha, anahakikisha bajeti inazingatiwa na kutoa ripoti za kifedha.

 

5. Msimamizi wa Itifaki & Mialiko ya Viongozi 
Anaratibu mialiko ya viongozi wa kitaifa, kimataifa, mabalozi, na wageni wa heshima.

 

6. Mshauri Mkuu wa Tamasha 
Anatoa ushauri wa kimkakati na kiitifaki, hususan kuhusu historia ya Afrika, viongozi, na maono ya Nyerere.


B). KAMATI NDOGO NDOGO ZA UTEKELEZAJI

 

1. Kamati ya Programu na Maudhui

2. Kamati ya Fedha na Rasilimali

3. Kamati ya Mawasiliano, Habari na Mahusiano ya Umma

4. Kamati ya Itifaki, Mialiko na Wageni Maalum

5. Kamati ya Makumbusho na Maonyesho ya Historia

6. Kamati ya Burudani na Sanaa 

7. Kamati ya utalii na Ziara za Kihistoria

8. Kamati ya Kliniki ya Afya na Huduma za Jamii                                                       

8. Kamati ya mafunzo ya Kiswahili (Tuseme Kiswahili)

9. Kamati ya Usalama na Logistics    

10. Kamati ya Tuzo 

11. Kamati ya Afya, Mazingira na Usafi 

 

 C). TAASISI ZITAKAZO SHIRIKISHWA KWENYE KAMATI (Kama wadau na washauri wa mambo ya kitaaluma)

 

 

  • “Kamati ya maandalizi itajumuisha wadau na washauri wa kitaalamu kutoka taasisi kuu za kitaifa na kimataifa zinazohusika na uratibu wa utamaduni, sanaa, lugha ya Kiswahili, urithi wa taifa, elimu ya juu, utalii, uhifadhi wa mazingira pamoja na ushirikiano wa kimataifa.”

Kuhusu sisi

Tamasha la Kimataifa la Julius Kambarage Nyerere (Tamasha la JuKaNye) Kuwaenzi Mashujaa na Wazalendo wa Kweli wa Afrika kupitia Urithi wa Julius Kambarage Nyerere. . Kukuza Uzalendo, Kuwawezesha Vijana na Kuimarisha Umoja kwa Maendeleo Endelevu.

Katibu Mtendaji wa Tamasha la Jukanye

CATZ COMPANY LTD

Mwandishi wa Tamasha la Kimataifa la Kimataifa la Julius Kambarage Nyerere (Tamasha la Jukanye)

Soma zaidi
id="wb_footer_a188dd9eef5301da18cbe22b97624cf4" class="wb_element wb-layout-element" data-plugin="LayoutElement">

ADDRESS:

P,O BOX  DAR- ES - SALAAM, TANZANIA

PHONE: +255 746 174403 +255 789  388232 +255 719 083050

EMAIL: jukanyefestival@gmail.com

info@jukanye.com

WEBSITE: www.jukanye.com