Kila T-shirt, Kofia na Kitenge ama bidhaa nyingine za Jukanye unazonunua ni zaidi ya vazi -
Ni heshima kwa mashujaa wetu, na mchango wako katika kuhifadhi na kuendeleza urithi wa Afrika kwa vizazi vijavyo.
Kwa kuvaa bidhaa za JUKANYE, unakuwa unaenzi urithi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na mashujaa wengine wa ukombozi wa Afrika.
Unaunga mkono Tamasha la Kimataifa la Julius Kambarage Nyerere (JUKANYE) na dhamira yake ya kuhamasisha, kuelimisha na kuunganisha Waafrika kupitia historia, utamaduni na urithi wetu.
Unachangia kufadhili programu za kuwawezesha vijana, kuhifadhi utamaduni na historia, kuimarisha umoja wa Afrika, na kuendeleza elimu ya historia kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
🔥Changia Tamasha. Nunua. Vaa. Jivunie. Changia JUKANYE.
